Jopo la Kiswahili ni la ange na ngangari laili wa nahari kuimarisha na kuboresha lugha ya taifa. Tunashughulikia kwa kina sarufi na insha ili kuhakiki kuwa wanagenzi wetu wamejihami vilivyo kwa ujuzi pamwe na maarifa ya kukabiliana na tamrini yoyote; masomoni au aushini. Kwa mukhtasari tumeweka msingi thabiti wa lugha hii tukufu katika mazingira aaliaali ya kumshawishi, kumvutia na kumnasa mwanagenzi yeyotekatika uhondo wake. Tunawalaki nyote ili tutopee na kubobea pamoja katika lugha ya Kiswahili. Kazole ya kheri.